MAJARIBIO BLOG

Saturday, June 29, 2013

MH. PINDA MGENI UKWAMANI JOGGING CLUB

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda, leo inasemekana anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Tamasaha la wana Ukwamani Jogging Club watafanya Tamasha lao katika Viwanja vya Tanganyika Packers huku zikihusisha Klabu mbalimbali za wana Jogging kutoka sehemu mbalimbai za Jiji La Dar s Salaam.


Ukwamani Jogging Club wakiwa katika picha ya pamoja
Taarifa kutoka kwa wana Jogging hao wa Ukwamani  lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kuelimishana juu masuala mbalimbali yanayomsababishia kijana kujikita katika vitendo viovu kama vile utumiaji wa madawa ya kulevya, wizi, Ujambazi n.k.

Wakati huo huo Jumapili iliyopita wana Jogging kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam walionyesha umoja wa hali ya juu baada ya kuhudhuria katika msiba wa mwana jogging mwenzao Amina Maarufu kama Herena Michael aliyefariki baada ya kugongwa na gari wakati akiwa na wenzake katika mazoezi ya kukimbia kutoka Mwananyamala kwa Kopa kwenda Coco Beach.

katika ajali wengine walinururika na wengine ni majeruhi akiwemo Maliki Doza aliye vunjika Kiuno, Taya na amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili, na Mwingine ni Mkuye ambaye alivunjika Miguu na kuwekewa Vyuma, Amina Bonge aliyepgwa kioo cha  site mirel ya gari hilo ambao hao ameruhusiwa.

miongoni mwa wana Jogging hao waliohudhuria katika msiba ni pamoja Ukwamani Jogging Club kutoka Kawe, Temeke kata ya 14, Msasani Joongging, Musfini Jogging, Vegas Jogging, Mwananyamala Jogging,
 Kunduchi Jogging, na nyinginezo.

wakazi kutoka sehemu mbalimbali wakimzika Herena Michael




 Picha mbali za wana Joggin waliohudhuria katika msiba wa Herena Michael



















PICHA NA MWANNE OTHMAN KUPITIA SIMU YAKE YA MKONONI


























No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine