MAJARIBIO BLOG

Monday, June 11, 2012

MPENZI CHOCOLATE YA JAHAZI LIVE TRAVELTINE

 

 MPENZI CHOCOLATE YA JAHAZI LIVE TRAVELTINE

       .Watasindikizwa wa wasanii wa Bongo Flava

Kundi la muziki wa taarab la Jahazi linatarajia kuzindua vidio ya albam yake juni 24 mwaka huu katika ukumbi wa Traveltine Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam

 Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi katika ofisi za East Africa Radio hivi karibuni Mkurugenzi wa kundi hilo Mfalme Mzee Yussuf, alisema albamu imejaa mapinduzi makubwa hasa katika wimbo uliobeba albamu hiyo ambao ni Habibt Roho Mpenzi Chocolate ulioimbwa na yeye mwenyewe.

Alisema vidio hiyo aliyoshuti katika mandhari tofauti hapa nchini Tanzania itakuwa ikimuonyesha  akiwa ndani helikopta na sehemu nyingine akiigiza kama mfalme wa kweli.

 "Nimetumia shilingi milioni nane za kitanzania kwa ajili kutengeneza vidio ya wimbo mmoja wa mpenzi chocolate lengo likiwa kuonyesha tofauti kati ya vidio zote zilizotangulia pia tunahitaji kuwa bora kimataifa"m alisema Mzee Yussuf.

Hivyo Mfalme aliwaomba wapenzi na mashabiki wa muziki huo kujitokeza kwa wingi kushuhudia laive bila chenga uzinduzi wa vidio hiyo  utakaosindikizwa na wasanii wa Bongo Flava sambamba na kupata burudani ya nyimbo mbalimbali kutoka kwao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine