MAJARIBIO BLOG

Friday, August 10, 2012

TANZANIA MOTO KUMKANA DAKTARI WA MAPENZI

Kundi la Muziki wa Taarab Tanzania Moto lililo chini ya ukurugenzi wake Amini Salmini linatarajia kutoa albamu zake mbili kwa mpigo huku zikisheheni nyimbo mbalimbali zinazotarajiwa kuwashika mashabiki wa tasnia hiyo.

Akizungumza na Tam Tam za Mwambao nyumbani kwake Mikocheni hivi  karibuni Amini alisema kuwa miongoni mwa nyimbo zitakazokuja kuleta ushindani katika kundi hilo ni pamoja na Hakuna Daktari wa Mapenzi, Nyuma ya Pazia na nyinginezo ambazo hakutaka kuzitaja.

Alisema wimbo huo wa Hakuna Daktari wa mapenzi unatarajiwa kuimbwa msanii machachari kutoka Zanzibar Nassoro Husein almaarufu 'Cholo' wakuta nyuma ya pazia utaimbwa  na Nyawana msanii ambaye wali alitoka kama msanii huru huku akitamba na wimbo Nipo Kamili Nimejipanga.

Naye Msanii nguli wa kundi hilo Joha Kassim ambaye pia ni mchumba wa Mkurugenzi huyo alisema kwa upande wake mashabiki watarajie vitu vikali kutoka kwake ambavyo kwa namna ama nyingine vitakonga vyoyo zao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine