MAJARIBIO BLOG

Friday, September 7, 2012

BI KIDUDE AENDELEA VIZURI HOSPITALI

Msanii nguli wa muziki wa taarab Fatma Baraka maarufu Bi Kidude imeelezwa kuwa hali yake inaendea vizuri huko alikolazwa katika hospitali ya Hindu mandali iliyopo jijini Dar  es Salaaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kundi Jahazi Morden Taara Mfalme Mzee Yussuf ambaye pia ni mjukuu wa Bi Kidude alisema hali yake inaendelea vizuri na jana (Alhamisi) alitoka kufanyiwa vipimo hivyo ataendelea kuwepi Hospitalini hapo mpaka pale hali yake itakapokuwa nzuri zaidi.

Mfalme akizungumza kuhusu kama anazungumza alisema kuwa hajapewa nafasi ya kuzungumza kutokana na hali inahitaka kupata mapumziko zaidi hivyo kumzuia kuongea. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine