MAJARIBIO BLOG

Thursday, December 13, 2012

JAHAZI KUIZINDUA WASI WASI WAKO DISEMBA 30

JAHAZI KUIZINDUA WASI WASI WAKO DISEMBA 30


Kundi la muziki wa taarab Jahazi lenye maskani yake jijini Dar es Salaam lililo chini ya Ukurugenzi wake Mfalme Mzeee Yussuf 'Big Daddy' mzee wa mafuta  linatajia kufanya uuzinduzi albam yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Wasi wasi wako ndo maradhi yako', utakaofanyika katika ukumbi wa Traveltine jijini Dar es salaaam.

Akizungumza na  mtangazaji wa kipindi cha Tam Tam za Mwambao kinachorushwa kila jumapili east africa radio  hivi karibuni Mfalme alisema uzinduzi huo utakuwa ni wa kipekee kwakuwa bendi yake imetoa nafasi vikundi vilivyo chini yake kuomba kuusindikiza uzinduzi huo.

Alisema  kwa kiingilio cha shilingi 20 tu wapenzi wataburudika kwa nyimbo mpya zitakazopatikana katika albamu hiyo mpya na bila kusahau zile za zamani ambapo alizitaja nyimbo mpya ni pamoja na wasi wasi wako ndo maradhi yako iliyobeba albamu muimbaji akiwa yeye mwenyewe, Mja wa Stara itakayoimbwa na chipukizi Rahma Machupa, Hata Bado Hujanuna na nyinginezo ambazo waimbaji wake ni pamoja Malkia Leila Bint Rashid, Muohammed Ally Mtoto Pori na Khadija Bint Yussuf.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine