- Ni katika Ukumbi wa Traveltine Magomeni
NA MWANNE OTHMAN.
Kundi la 5stars Morden Taarab a.k.a Watoto wa Bongo Jumamosi ya wiki hii wanatarajia kuvamia Ngome ya Jahaz Morden Taarab Wana wa Nakshi Nakshi Traveltine Hotel Magomeni, kwa kufanya shoo yake ya kwanza mara baada ya kuzinduliwa kwa bendi hiyo mnamo April 27 mwaka huu.
kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kundi hilo Maalim Sharif Mango marufu kama Sharks onyesho hilo litakuwa la kwanza toka kuzindua kwa bendi hiyo sambamba na albam yao ya Ukurasa Mpya wimbo ulioimbwa mpiga kinanda Ally J. MAARUFU Baba Rujaina.
5stars ambayo itashuka ukumbina hapo mara baada ya kurejea katika safari yao ya Mikoani walikokwenda kuizindua albam yao hiyo sambamba na kutambulisha bendi hiyo iliyo chini ukurgenzi wake Sharks, ikiwa na waimbaji wake nguli katika Tasnia ya Taarab akiwemo Mwanahawa Ally, Sabah Salum Muchacho, Mwamvita Shaibu, Zena Mohammed, Mosi Suleima n, Maua Tego na chipkizi kibao. wakati katika safu ya wapigaji akiwemo mpiga kinanda Thabit Abdul, Ally J ambaye pia muimbaji, Rajab Kondo na wengineo.
Miongoni mwa vibao ambavyo wanavitarajia kukonga mashabiki wake ni pamoja Muomba Mungu hatoki Mtupu, Ukurasa Mpya, Mwenye Hila, La uchungu na nyingine nyingi mpya na za zamani.
Sharks aliwataka wapenzi na mashabiki wa 5stars kujiandaa mkao wa kula kwani onyesho hilo litakuwa ni moto wa kuotea mbali.
![]() |
Mwimbaji aliyeimba wimbo uliobeba jina la albam mpya ya 5stars inayokwenda kwa jina la Ukurasa Mpya Ally J. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine