Mwimbaji wa kundi la Jahazi Morden Taarab Fatma Mahmoud aka Mcharuko amesema hana mpango wa kuacha bendi yake ila hatokuwepo jukwaani kutokana na likizo ya uzazi.
Akizungumza na mtangazaji wa Tam Tam za Mwambao kipindi cha taarab kinachorushwa East Africa Radio alipokwenda kumtembelea nyumbani kwao Magereza Visiwan Zanzibar Fatma ambaye pia amejifungua mtoto wa kike mnamo mwezi wa tatu alisema hana mpango wa kuacha bendi yake kwa kuwa hana sababu ya kuacha.
"Akaaa sina mpango wa kuacha bendi mie manake kama mshahara nalipwa kama kawaida nioachie nini? wanaosema na waseme alisema Fatma Mcharuko.
aidha aliwataka wapenzi wake kuwa na subira naye na wamvumilie katika kipindi chote cha ulezi mpaka mtoto wake atakapofikia wakati wa yeye kuanza kazi.
aidha alipotakiwa kutaja ni msanii gani ambaye yeye anamuhofia kwa upande wa kwao Zanzibar ambaye yupo katika rika lake yeye kimuziki alisema hatishiki na mwimbaji yeyote ambaye yupo katika rika lake kimuziki kwakuw anajiamini anajua.
Fatma Mahmoud kati kati akiwa na wacheza viduku wa bendi ya Jahazi wakifanya vitu vyao stejini |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine