Friday, June 28, 2013
KINGS YAMDAKA SALHA WA HAMER Q
Baada ya Dar Morden kumwaga Salha Abdallah maarufu kama Salha wa Hammer hatimaye bendi ya Kings Morden Taarab chini ya Ukurugenzi wake Majaliwa ameamua kumdaka ili kujiunga na kundi lake
imefahamika.
Akizungumza leo kwa njia ya simu na mwandishi wa habari Salha alisema tayari alishakutana na Mkurugenzi huyo na tayari walishazungumza kwahiyo anasubiri maamuzi kutokana na makubaliano hayo.
"Ni kweli wamenihitaji na tayari nieshazungumza nao lakini bado hatujafikia muafaka ila iwapo kama wataafiki matakwa yangu basi nitakuwa miongoni mwam wasanii wa Kings" alisema Salha
Salha ambaye alikuwa ni msanii wa kikundi cha taarab ya Kiasa cha Dar es Salaam alifukuzwa katika bendi hiyo kwa kosa la kurekodi wimbo nje ya Bendi ambapo wimbo huo aliimba yeye na mumewe Hammer Q, na kwa sasa wako mbioni kukamilisha albam yao itakayopkwenda kwa jina Mke na Mume.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine