MAJARIBIO BLOG

Friday, June 28, 2013

MZEE MAJUTO AMLETA PUNDAMILIA


MCHEKESHAJI Nguli Nchini Tanzania King Majuto amesema yuko mbioni  kutoa filam yake mpya itakayokwenda kwa jina la Zebra.
King Majuto
akizungumza na mwandishi habari hii katika Hoteli ya Itumbi iliyopo Mwembe Chai  jijini Dar es Salaam King Majuto alisema lengo la kuipa jina la Zebra filamu yake hiyo ni kwamba ana lengo la kutoa elimu ya maana ya mistari ya pumndamilia iliyochorwa barabarani.

Alisema sababu iliyopekelea hadi kutaka kutoa elimu juu ya mistari hiyo ni kwamba alishuhudia ajali iliyotokea Ilala pale dereva wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda alipomgonga mtoto na kumburuza kiasi cha umbali wa mita kumi na hatimaye kumsababishia kifo mtoto buyo.

"Nilikuwa natoka msikitini majira ya saa kumi adhuhuri nilikuwa nimekaa katika kibaraza cha msikiti huo ambao upo kando kando ya barabara ambapo nilimshuhudia mtoto kwa macho yangu akigongwa na kufa hapo hapo wallah sikuweza kwenda kuendelea na kazi siku ile ambapo nilikuja Dar kwa lengo la kurekodi filamu ya Nakwenda kwa Mwanagu niliyoigiza mimi na JB" alisema Mzee Majuto.

Aidha alisema wapenzi wa sanaa ya maigizo wajiandae kulia machozi kwasababu filam hiyo itakuja kugusa mioyo ya watu, ambapo alisema kuwa anafikiria kuingizia na nyimbo mfano kama wa filam za Kihindi lakini anahofia atawaliza zaidi wapenzi wake.

 


No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine