![]() |
Marehemu Jafarry Ally enzi za uhai wake |
Akizungumza kwa njia ya simu na mmiliki wa blog hii Khadija Kopa alisema tukio hilo lilitokea majira ya usiku wakati alipokuwa amelala nyumbani kwake hapo alipokuwa akiishi na marehemu mumewe ambapo wezi hao walibanua dirisha la aluminiaum ambalo alisahau kulifunga na hatimaye wezi hao kufanikiwa kuchomoa mkoba ambao ulikuwa karibu na dirisha hilo.
Akizungumzia kuhusiana na arobaini hiyo alisema inatarajiwa kuftarisha huku ikiambatana na kisomo kitakachosomwa kabla ama baada ya Futari.
Akizungumzia kuhusu iwapo atahama kwenye nyumba ya marehemu mumewe kwa sasa Khadija kopa ambaye kesho atamaliza arobaini ya mumewe huku akiendelea kukaa EDA alisema ataendelea kukaa hapo mpaka atakapomaliza EDA na bada ya hapo bado hajajua atakwenda kuishi wapi ingawa wakwe zake walimwambia aendelee kuishi hapo.
![]() | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Khadija Kopa akilia kwa chungu mara baada ya kupata taarifa za msiba wa mumewe |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine