MAJARIBIO BLOG

Thursday, July 18, 2013

JUMA MGUNDA HATIMAYE AMEZIKWA LEO MKAMBA

NA MWANNE OTHMAN

Aliyekuwa Mpiga Gitaa la Base wa kundi la Jahazi Morden Taarab Juma Mgunda aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, hatimaye amezikwa leo katika kijiji cha Mkamba Mkulanga, imefahamika.

Kwa Mujibu wa ndugu wa marehemu Juma Mgunda aliyejulikana kwa jina la Mgeni Saidi ambaye pia ni mpiga kinanda wa Jahazi alisema marehemu Juma alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kifua Kikuu kwa muda mrefu mara baada ya kuacha bendi ya Jahazi, ambapo aliwahi kutumua dozi na kumaliza.

mwili wa marehemu Juma Mgunda ukiwa ndani ya sanduku tayari kwa kusafirishwa

 Alisema baada ya kupona na kujiona yuko imara akajikuta akirudia kazi zake ngumu za kufanya muziki kusafiri na bendi kama 5stars , na ujana nao akajikuta hali hiyo ya ugongwa ikimrudia kidogo kidogo, huku akiendelea na shuhuli zake, lakini hivi karibuni hali yake ilizidi kuwa mbaya na hatimaye hadi kufikia jana kuiaga dunia.


 mwili wa marehemu Juma Mgunda ukiwa ndani ya sanduku tayari kwa kusafirishwa


Mtangazaji wa east africa radio na EATV Mwanne Othman akimuhoji mpiga kinanda wa Jahazi Chid Boy

Juma Mgunda kabla ya kuingia Jahazi aliwahi kutumikia kikundi cha Tanzania One Theter yaani TOT na baada ya hapo kwenda Jahazi ambapo alipata kurikodi albam ya Daktari wa Mapenzi iliyozidi kumuongezea umaarufu kwa kujulikana kama Juma Mgunda Jino Moja.

Shuhuli za mazishi hayo yaliyohudhuriwa na wasanii wa bendi mbalimbali za Taarab na wa maigizo zilianzia nyumbani kwao Tandika na ilipofika saa 5 asubuhi mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea Mkamba tayari kwa maziko.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU JUMA MGUNDA AAAMIN.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine