MAJARIBIO BLOG

Tuesday, September 17, 2013

AHMED MGENI HATIMAYE AFARIKI DUNIA

-Alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kifua Kikuu,
-Wapenzi wa taarab watamkumbuka kwa nyimbo na Utanashati wake

 Na Mwanne Othman

 MWIMBAJI wa Taarab Ahmed Mgeni amefariki dunia usiku wa kuamkia leo ambapo mazishi mpaka sasa yanaendelea kufanyikia nyumbani kwao Aman Fresh Zanzibar na atazikwa  majira ya saa 10 jioni katika makaburi Mwanakwerekwe Visiwani Humo. Kwa Mujibu wa dada wa Marehemu Laithat Mgeni kwamba Ahmed Mgeni alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Tyfod na Kifua Kikuu kwa takriban miezi mitano mpaka kufikia sasa umauti wake.
 Marehemu Ahmed Mgeni enzi za Uhai wake

Ahmed Mgeni aliingia katika tasnia ya Taarab mnamo mwaka 2000 ambapo kikundi chake cha kwanza kilikuwa ni Nady Ikhwan Saafaa kilichopo Zanzibar na baadaye kuja Dar es Salaam na kuhamia katika kundi la Zanzibar stars Morden Taraab ambapo alipata kurikodi wimbo wake wa kwanza uitwao MSITUBUGUDHI, TWAJIFARAGUA KWA RAHA ZETU na nyinginezo.

 Mnamo mwaka 2010, Ahmed Mgeni aliamua kuanzisha kundi lake lililoitwa Zanzibar Njema Morden Taraab ambapo hapo alipata kutoa albam yake ya kwanza iliyobeba jina la KITCHEN PATRY NAMBA 2, na albam yake ya pili ni SITETEREKI ambayo bado inaendelea kufanya vizuri mpaka sasa.

 Na kwa mujibu wa Laithat Mgeni ni kwamba Ahmed Mgeni alizaliwa mwaka 1984, elimu yake ya msingi aliipatia katika shule ya msingi Kisiwandui wakati Sekondari aliipatia katika shule ya Hailesasi zote za huko huko Zanzibar. MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU AHMED MGENI MAHALI PEMA PEPONI.

Picha mbalimbali za waliohudhuria msiba wa Ahmed Mgeni Huko Zanzibar
hawa ni baadhi ya watu waliohudhuria katika msiba wa Ahmed Mgeni huko Zanzibar









No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine