MAJARIBIO BLOG

Thursday, October 10, 2013

EATV NA EA RADIO KUWALETA P SQURE NCHINI

Na Mwanne Othman

Wasanii wakali na machachari Africa ambao ni Mapacha Peter na Paul maarufu ' P Squre' wanatarajiwa kuja nchini Tanzania na kufanya shoo kali na kabambe jijini Dar es Salam mnamo tarehe 23 Mwezi wa 11 mwaka huu 2013.

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency zamani Kempiski jijini Dar es Salaam Mtangazaji wa East Africa Television pamoja East Africa Radio ambao ndio waratibu wa Tamasha hilo, Hilaly Daudi maarufu Zembwela alisema kuwa lengo kubwa la kuwaleta wanamuziki hao wanaoongoza kwa umaarufu kila kona Duniani ni kutoa Burudani na Somo kwa wanamuziki wa Tanzania kwa namna ambavyo muziki unaweza kufanyika katika hali tofauti na waliyozoea.

p squre wakiwa katika pozi

Mapacha wawili wakiwa katika pozi
Zembwela alisema Tamasha hilo litakuwa ni la moja kwa moja kutoka kwenye ala ambapo kwa lugha ya Kigeni tunaita Live Band na jumla ya wanamuziki 13 wataambatana na P squre kufanya shoo hiyo.

P squre watafanya onesho masaa mawili mfululizo bila kupumzika na kutakuwa na wasanii wa kuwasindikiza ambao tutakuwa tunawatangaza kadri muda utakavyozidi kukaribia “ alisema Zembwela.

Tamasha hilo la Kihistoria limedhaminiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania ambao wamekuwa wa kwanza kuonesha ushirikiano katika hilo na wamekubaliana na Waratibu ambao ni EATV na East Africa Radio kuifanikisha Burudani hiyo kubwa na ya aina yake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine