KISA...................... SOMA HABARI KAMILI
NA MWANNE OTHMAN
Msichana
wa kazi katika nyumba moja iliyopo Mbagala kwa Mangaya anayefahamika
kwa jina la Sailis Mapunda mwenye umri wa miaka 18 amejeruhiwa vibaya
kwa Viwembe na wanawake wawili ambao wanaosemekana kuwa ni mtu na mke
mwenzie, imefahamika.
Akizungumza
Mwanne Othman huko nyumbanin kwao Mbagala kwa Mangaya, Sailis
alisema kuwa wanawake hao alikutana nao njiani akitokea dukani
kununua mkate ambao walimsimamisha na kumuuliza kuwa wewe ndo Salome
na kuwajibu haha kwamba yeye si Salome.
![]() |
SAILIS AKIWA AMEUMIA USONI BAADA YA KUPIGWA KWA MADAI YA KUSINGIZIWA SKENDO |
Alisema
wanawake hao hawakutaka kumuamini Sailis hivyo waliendelea kumsakama
na kumtuhumu kwamba ndo Salome anayewachukulia mume wao na kuanza
kumvamia mmmoja akimpiga na mwengine kumkata VIWEMBE katika sehemu
mbalimbali za mwili ikiwemo Usoni karibu kabisa na Jicho, Mgongoni
pamoja na Mikononi hatimaye kumsababishia maumivu makali.
Sailis
alisema wanawake hao ambao ambao majina yao yapo kapuni wakiwa
na umri kati ya miaka 24 na 25 kwamba hawajui na hakuwahi kukutana
nao awali.
Mpaka
sasa kesi iko kwenye Vyombo vya Dola.
![]() |
HAPA AKIWA NA SHANGAZI YAKE PAMOJA NA DADA ZAKE. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine