KHADIJA
KOPA KUTOKA EDA
Mwimbaji
wa muziki wa taarab ya Kisasa maarufu Malikia wa Mipasho Khadija Omar
Kopa anatarajia kutoka Eda Tarehe 13 mwezi huu wa 10, sawa na siku
ya Jumapili huko nyumbani kwa Marehemu Mumewe Jafar Ally Bagamoyo.
Akizungumza
na Mwanne Othman kwa njia ya simu Khadija Kopa alisema anatarajia
kumaliza eda yake hiyo siku ya tarehe 13 lakini nje atatoka rasmi
siku ya tarehe 14 yaani Jumatatu ijayo ambapo alisema angependa
kusomewa Dua ili Mwenyezi Mungu amzidishie Moyo wa Iman.
![]() |
KHADIJA KOPA SIKU ALIYOFIWA NA MUMEWE |
Khadija
Kopa alikuwan ndani kwa Takriban miezi minne na siku 10 baada ya
kufiwa na mumewe aliyekuwa Diwani wa Kata ya Magomeni Wilaya ya
Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo alifariki dunia mnamo mwishoni mwa mwezi
wa tano akisumbuliwa na maradhi ya malaria na alizikwa katika
makaburi yaliyopo Magomeni wilaya ya Bagamoyo Mkoani humo, huku
akimuacha Mkewe Kipenzi Khadija Kopa kwenye EDA, akiwa katika wakati
Mgumu wa kumkosa mumewe kipenzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine