Na
Mwanne Othman
Baadhi
ya madereva wa daladala jijini Dar es Salaam wamesema hatua
inayotarajiwa kufanyika ya kufutwa kwa njia 64 za daladala ili
kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam,
itawaathiri kwa kisasi kikubwa kikazi kwani asilimia kubwa ya abiria
hupatikana katika njia hizo, Ea Drive imezungumza nao.
Nilizungumza
na Mshauri Elekezi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dae es Salaam ndugu
Felix Mlaki ambaye naye kwa upande wake alielezea mpango mzima
uliosababisha hatua hiyo kufikiwa ni kwamba lengo ni kutoa nafasi kwa
mabasi hayo pindi yatakapoanza na madaladala yatapatiwa njia mbadala
kutoka SUMATRA.
Aidha
alisema wananchi watarajie kutopata usumbufu katika safari zao kwani
wana mfumo mzuri katika ununuzi wa tiketi unaweza kununua tiketi ya
hata ya wiki nzima, na kufika safari yake bila kuchelewa
Akizungumzia
juu ya nauli ya usafiri huo alisema kuwa wapo katika mchakato wa
kukokotoa na utakapomalizika mchakato huo watatoa taarifa kamili.
Ndugu
Mlaki akizitaja barabara hizo zitakazoathirika ni pamoja na Kariakoo
Mwenge, Posta Mwenge, Ubungo Kariakoo, Mbezi na kadhalika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine