Kambi ya Kampuni ya holtan
iliyoko katika eneo la Jangwani iliyopewa tenda ya kutengeneza vituo
vya mradi wa mabasi yaendayo kasi imepatwa na hasara kubwa kwa
upotevu mali zilizokwenda na maji baada ya Mvua kubwa zilizonyesha.
Wakizungumza na East
Africa Drive wahusika wa mradi huo ambaye mmoja yeye ni msimamizi wa
mradi anayefahamika kwa jina la ndugu: Jamal na Injinia George Ocheni
ambaye yeye ni Meneja Mradi, walisema kutokana na maafa hayo
yaliyotokea kuna uwezekano mkubwa wa shuhuli za ujenzi wa vituo hivyo
vikapungua kutokana kwa sasa wapo katika hatua ya kuokoa mali
zilizosalia.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine