Na Mwanne Othman
15/5/2014
Shirika
la maji safi na maji taka Dawasco limefanikiwa kukamata zaidi ya watu
watano katika oparesheni yake iliyoanza jana inayolenga kuwasaka
wahujumu wa shirika hilo wanaojiunganishia maji kinyume na sheria.
Akizungumza
na mwanneothman.blogspot.com, Msemaji wa Dawasco Everlasting Lyaro
amesema oparesheni hiyo ni kuduma na kusema wamesikitishwa na mbinu
walizogundua jinsi mtu mmoja anavyoweza kudhulumu haki za wenzake za
kukosa maji takriban miezi mitatu.
Aidha
Bi Everlasting ametoa wito kwa wananchi kuonesha ushirikiano kwa
Dawasco kwa kutoa taarifa pindi wanapoona kuna mtu anakwenda kinyume
na sheria katika kuhujumu Shirika hilo, pamoja na kuanisha vitu
walivyokama kama wahujumu hao na kutolea mfano kuwa huu ni ujangili
pia, kwani ujangili si kwa wanyama pori pekee hata wahujumu maji
wanawahesabia pia ni majangili.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine