Na Mwanne Othman
15/5/2014
Majambazi
watatu wameuwa na wananchi wenye hasira kali na wengine wawili
kujeruhiwa vibaya huko Mkoani Mbeya wakati wakifanya Jaribio la
Utekaji mali tukio lililotokea kijiji cha Mshangamwelu Kata ya Njewe
Walaya ya Chunya Mkoani Mbeya katika Barabara ya Mbalini
kuelekeaMkwajuni.
Kwa
Mujibu wa Kamanda Polisi Mkoani Mbeya KamandaAhmed Msangi alisema
tukio hilo lilitokea majira ya usiku ambapo majambazi hao waliokuwa
watano waliweka mawe na Magogo barabarani ili kwa lengo la kutaka
kukamata magari kwa urahisi ili waweze kufanikiwa kazi yao kwa
urahisi.
Kamanda
Msangi pia alifahamisha jinsi majambazi wengine wawili walivyoweza
kupatika siku ya pili yake wakifanya jaribio la kutoroka eneo hilo
ambapo amesema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Msangi akizungumza na
waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani).
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine