MAJARIBIO BLOG

Friday, May 23, 2014

USIKOSE TAM TAM ZA MWAMBAO KILA JUMAPILI

Usikose kusikiliza Tam Tam za Mwambao kipindi cha taarab kinachokujia  kila siku za Jumapili kuanzia saa 4 hadi saa 6 mchana ndani ya east africa radio ukiwa na Mwanne  Bint Othman aka toto la Matashtit.

MWANNE TOTO LA MATASHTIT AKIFANYA YAKE

Hapo utapata kusikia nyimbo za taarab ya zamani katika kipengele cha 'TUNAKUMBUKA ZAMANIII'.

MWIMBAJI WA TAARAB ASILIA KUTOKA ZANZIBAR MOHAMMED ILYAS

UKIUSIKIA MUHOGO WA JANG'OMBE HUTOKOSA KUMTAJA MAREHEMU BI FATMA BINT BARAKA MAARUFU BI KIDUDE
 Lakini pia katika Kipengengele cha Afya utamkuta mtaalam wa magonjwa ya mfumo wa uzazi kwa wanawake na wanaume kutoka Foreplan Clinic hapa namzungumzia Dr. Mwaka akitupatia ushauri wa jinsi gani ya kujikinga na magonjwa mbalimbali, na kutufahamisha kuwa nini sababu za magonjwa hayo, dalili pia, kinga na maana ya magonjwa mbalimbali.


DR. MWAKA AKISISITIZA JAMBO

Bila Kusahau katika KIJAMVINI hapa utasikia habari mbalimbali kuhusiana na wasanii wa taarab aidha udaku au za kimaendeleo.

Lakini pia Bila kusahau Bandika Bandua ya Muziki huo wa taarab hapo ni kuachia bodi, kidole kwenda kwa mbele
MASHAUZI CLASSIC WAKIWA STEJINI





EAST AFRICA MELODY WAKIWA STEJINI

JAHAZI WAKIWA STEJINI


DAR MORDEN WAKIWA MAZOEZINI WALIPOKUWA WAKIJIANDAA NA UZINDUZI WAO ULIOPITA

FUNGA KAZI
T MOTO NDANI YA STEJI

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine