BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE AAMIN
Alikuwa ni msanii wa Bongo Movie ambaye amefariki leo alipokuwa akijifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa Rais wa Bongo wa Movie Steven Nyerere marehemu alijifungua mtoto na baada ya muda mfupi mtoto alipoteza maisha huku marehemu Recho akiwa na hali mbaya ndipo walipomuhamishia ICU lakini kutokana na mipango ya Mungu naye alifariki dunia.
Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ndugu Kaftany ni kwamba wasanii wote wanatakiwa kukutana katika viwanja vya leaders klabu kwa ajili ya mipango ya mazishi ya mpendwa wao Recho haule
![]() |
MAREHEMU RECHO ENZI ZA UHAI WAKE |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine