Na Mwanne Othma
Vijana nchini wametakiwa
kutambua umuhimu wa kushiriki katika chaguzi ndogo hususan chaguzi za
Serikali za Mtaa ili kujiongezea uelewa zaidi katika kufahamu mambo
muhimu yanayoambatana na chaguzi hizo.
Akizungumza na Drive
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwananyamala kwa Kopa ndugu Juma
Mbilinga amesema vijana wengi na hata baadhi ya Wazee wamekuwa
wakidharau chaguzi za Serikali za Mitaa bila kujali kwamba Serikali
huanzia katika ngazi hiyo.
Aidha Drive ilizungumza na
Vijana wenyewe iwapo wana uelewa na kufahamu umuhimu wa kushiriki
katika chaguzi ndogo ndogo hususan Serikali za mitaa ambapo walisema changamoto ya maeneo ya kupigia kura, uchache wa vifaa hali inasababisha kijana kukaa muda mrefu kusubii kupiga kura huchangia vijana kutoshiriki kikamilifu..
Kadhalika tulizungumza na
Mama Ukoko Zigo kama mzazi akizungumzia iwapo wazazi wanachangia
kuwazuia watoto wao kutoshiriki katika harakati hizo za uchaguzi
ambae nae kwa upande wake alisema yuko katika mstari wa mbele katika kuwahamasisha vijana kushiriki.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine