Abbas Shentemba Mzee wa Cash money anakuletea shoo maalum ya kukata na shika itakayobebwa na Kundi zima la Mashauzi Clasic chini ya Ukurugenzi wake Isha Ramadhani itakayofanyika Juni mosi katika Ukumbi wa Traveltine Hotel Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Abbas Shentemba shoo yenye kiingilio cha shilingi elfu 5 tu, itasindikizwa na wasanii kibao akiwemo Bi Shakira Said, Afua Suleiman Kutoka Gusa gusa, Ustadh Mohammed, Kibao kata, Juma Bhalo wa Tanzania bila kuwasahau kanga Kanga moja wakiwa katika muonekano mpya kabisa.
Shentemba amesema pia kutakuwa na zawadi kwa watu 300 wa mwanzo wataapata bia moja bure na zawadi la laki moja (100,000) itatolewa na mzee wa Cash Money.
Imedhaminiwa na Airtel, Konyagi, Redd's na Cash Money No Change.
TAZAMA PICHA WASANII WATAKAOKUWEPO JUNE 1, NDANI TA TRAVELTINE HOTEL MAGOMENI
![]() |
ISHA MASHAUZI AKIWA STEJINI AKIFANYA VITU VYAKE |
![]() | |||
AFUA SULEIMAN |
![]() | |
BI SHAKILA SAID |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine