Na Mwanne Othman
Waziri
wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh. Feneral Mukangara
amewaomba wasanii wa tasnia ya filamu nchini wasimamie kazi zao
ipasavyo kuhakikisha wanajijengea mfumo chanya katika kazi zao, huku
wakijewekea utaratibu wa kwenda hospitali kuangalia afya zao ili
kujiepusha na magonjwa nyemelezi.
Mh.
Waziri Fenera ameyasema hayo jana katika viwanja vya leaders klabu
katika shuhuli za kuagwa kwa msanii wa filam Adam Philip Kuambiana
ambaye amezekwa leo mchana katika makaburi ya Kinondoni.
Aidha
akijibu swali la mmoja wa wasanii anayefahamika kwa jina la Dr. Cheni
la kuomba wasanii wa filamu kutengewa eneo ama kiwanja chao maalum
cha kuzikiwa ambapo alisema.
![]() | |||
Waziri Habari Vijana Utamadunin na Michezo |
![]() |
Mh. Waziri Mukangara akiwasili katika viwanja vya leader club wakati wa shuhuli za kuaga mazishi ya marehem Adam Kuambiana |
Kadhalika
Mstahiki Meya wa Kindondoni ndugu Yussuf Mwenda alisema ameguswa sana
msiba huu kwani licha Adam kuambiana kuwa msanii lakini pia ni mmsiba
wa mwanaharakati mwenzao katika kulitumikia Taifa akiwa na maana ya
kwamba ni msiba unaomuhusu Diwani wa Kunduchi Mh. Janeth Rite ambaye
ndiye mke wa Marehemu.
Naye
Rais Bongo Movie Steve Nyerere kwa masikitiko makubwa aliwataka
wasanii wa tasnia hiyo kuacha majivuno na badala yake kuwa na
mshikamano na upendo kutokana na hakuna mtu ambaye anaijua siku yake
ya kutangulia.
Na
hii ni nukuu ya Mh. Janeth Rite akimoboleza kwa kusema “ooohh Mume
wangu, nakupenda mume wangu, Mungu mpokeee mume wangu Adam, sauti ya
mume wangu adam, mpambanaji wangu, askari wangu, nani ataniita my
permanent intrest” alisema maneno hayo huku akilia kwa uchungu.
![]() | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Mke wa marehem Adam Kuambia ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kunduchi Mh. Janeth Rite akimuaga mumewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi aaaaami. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine