MAJARIBIO BLOG

Wednesday, July 2, 2014

Na Mwanne Othman

Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhwani Jakaya Kikwete amekiri kuwaita baadhi ya waandishi wa habari ni makanjanja na kusisitiza kutowaomba radhi waandishi juu kauli hiyo, na kuiomba tasnia ya habari kuitumia kalamu yao katika kuandika habari zenye uhakika na si kuitumia kama kisu ama bunduki kutisha watu.

Mh. Ridhwani ameyasema hayo alipokuwa akizungumzi kauli aliyoitoa hivi karibuni kwenye moja ya mahafali yaliyofanyika huko Morogoro ya kusema kwamba kuna baadhi ya waandishi wengine wa habari wana tabia ya ukanjanja.

Mh Ridhwani akiwa katika shuhukli zake za kiserikali

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine