Na Mwanne Othman
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Sinza ya jijini Dar es Salaam Dokta
Benedict Luwoga ametoa wito kwa wateja (wagongwa) ambao wana
uthibitisho wa malalamiko ya ya kutotendewa haki yanayoyotokana na
uzembe wa wafanyakazi wa hospitali hiyo ili hatua za kinidhamu
zichukuliwe juu yao.
Dokta
Luwoga ameyasema hayo baada ya hospitali hiyo kuripotiwa kwenye
gazeti kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoikabili hospitali yake juu
ya kumuacha mgonjwa mahututi kwa masaa mawili bila kumpatia huduma
ya aina yeyote.
Hapo
awali mmoja wa ndugu ambaye amempeleka mgonjwa wake alisema walinzi
pia wanachangia kukwaza ndugu wa wagonjwa ambao wakati mwingine
huhitajika kumuangalia mgonjwa wake kwa karibu hivyo kujikuta
wakifukuzwa na walinzi hap..
Aidha
Dr. Luwoga ameviomba kwa vyombo vya habari watumie fursa walizopewa
kuweza kuelimisha jamii na si kuleta migongano na kuharibu sifa za
vitengo vichache vya Serikali.
hospitali ya sinza katika picha |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine