MAJARIBIO BLOG

Friday, December 14, 2012

THABIT ABDUL KUMTENDA MWANAHAWA CHIPOLOPOLO

Yasemekana mwanahawa ni mja mzito
Thabit aikana, asema hajawahi kukutana naye
thabit Abdul akiwa katika pozi









Mwanahawa akiwa stejini











baada ya tashtit zote za mjini walizokuwa wakizonyesha kudhihirisha uhusiano kati ya wawili hao na Thabit Abdul ambaye ni mpiga kinada maarufu katika nyimbo mbalimbali za taaarab  na Mwanahawa Chipolopolo mwimbaji wa kundi la taarab la Kings,  hatimaye mwanakaka mtanashati aikana mimba ya Mrembo huo mwenye macho ya kuvutia kama mwanakaka huyo alivyokuwa akimfagilia.

thabit ambaye miezi kadhaa iliyopita ilisemekana kuwa alitomtolea barua ya uchumba bint huyo kwa lengo la kutaka kumuoa, ambapo pia aliwahi kuahidi katika kipindi cha Hotmix kinachorushwa na kituo cha televisheni cha EaTv  alipokuwa akifanya mahojiano kwamba Novemba mwaka huu angefanya maajabu makubwa sana kwa mpenzi wake huyo lakini baadaye ilikuja kufahamika kuwa angemvisha pete ya uchumba kitu ambacho hakikuwa mpaka sasa.

wakati thabit akiendelea kumkana Mwanahawa huku nako baadhi ya wadau wa taarab wamestukia ishu kwa kusema kuwa yawezekana wawili hao wamepanga mpango madhubuti kwa ajili ya kujifanyia promo kwa kuwa wameandaa albamu yao ya taarab. 


No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine