MAJARIBIO BLOG

Wednesday, February 13, 2013

ALLY J AIMBA TAARAB

-AFUNGUA UKURASA MPYA

Mpiga kinanda maarufu katika tasnia ya muziki wa taarab hapa nchini Tanzania anayetumikia kundi la 5tars Morden Taarab ambaye pia ndiye Rais wa kundi hilo  Ally J aka Ally Kemikali anatarajia kuimba muziki wenye mahadhi hayo, imefahamika.

akizungumza na Tam Tam za mwambao Ally J alisema kuimba anajua kwa kuzingatia kuwa nyimbo zote 5stars yeye ndiye muongozaji hizo ana jiamimni kuwa abnaweza ili muda na wakt ndo haujafika na utakapofika basi ataimba.

"Ukiangalia kama Mzee Yussuf yule pale anaimba japokuwa alikuwa mpiga kinada kama sisi lakini aliamua kuimba na mpaka sasa anaimba, kadhalika Thabit abdul naye pia ni mpiga kinanda alikana pia aliamua kuimba na ameimba hivyo nami wakati wangu ukifika basi nitaimba." alisema Ally J.

Aliutaja wimbo ambao atatoka nao katika tasnia hiyo  utakuwa katika mahadhi ya taarab ni unakwenda jina la Ukurasa Mpya.

Ally J  aliongezea kuwa wengi watajiuliza ukurasa mpya huu wa kuanza kuimba, au kampata mpenzi mpya lakini alisema jibu litapatikana hapo baadaye.



No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine