-Ni Aisha Vuvuzela, asema rizki popote
NA MWANNE OTHMAN
Mwimbaji wa Machachari wa kundi la taarab la Mashauzi Classic lililo chini ya ukurugenzi wake Isha Mashauzi anayekwenda kwa jina Aisha Othman aka mamaa Vuvuzela aikimbia bendi hiyo kwa madai ya kuchoshwa na madhila yaliyokuwa yakimkumba mara kwa mara.
Kwa mujibu wa msanii huyo alisema japo kuwa ameacha bendi hiyo lakini bado ataendelea kuipenda na kuipa ushirikiano wa karibu pindi pale atakapohitajika, kwa kuwa ana imani ameishi vizuri na wasanii pamoja na viongozi wake.
Akizungumzia kuhusu kufanya kazi na bendi nyinguine alisema atapumzika nyumbani wiki moja kwanza halafu ndio ataangalia mchakato wa kuazama wapi aende.
Aisha ambaye ni mwimbaji aliyekuwa akishikilia vema nafasi ya Mkurugenzi wake pind anapokuwa hayupo stejini na alikuwa kiraka katika nyimbo mbali mbali zilizoimbwa Isha kama vile Tugawane Ustaarab, Acheni Kuniandama na nyinginezo.
![]() |
Aisha Vuvuzela akiwa katika pozi |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine