Mwimbaji machachari wa kundi la Dar es Salaam Morden Taarab Salha Abdallah ambaye pia ni Mke halali wa Muimbaji wa kundi la 5stars Morden Taarab Hammer Q, amefukuzwa katika bendi hiyo kwa kosa la kuimba wimbo nje ya bendi yake imefahamika.
Kwa Mujibu wa Salha alisema wimbo huo ni ambao ameimba pamoja na mumewe mara baada ya kusameheana na kurejeana baada ya mtafaruku uliotokea wiki kadhaa zilizopita ambapo Hammer Q alimtwanga mkewe nusura amuue kwa tuhuma za wivu.
Salha ambaye mara nyingi amekuwa akituma ujumbe katika ukurasa wa facebook unaoashiria jinsi gani anampenda mumewe Hammer Q amesema hawezi kumkatalia mumewe kuacha kufanya naye kazi akizingatia itawaongezea kipato katika maisha yao na kwamba wote ni wasanii tena wenye fani ya taarab na miduara.
"Eti kisa nime rekodi wimbi na mume wangu ndo nimefukuzwa bendi, kurekodi wimbo na mume wangu haikumaanisha kwamba nataka kuacha Dar Morden hapana ila tunajitafutia riziki mimi na mume wangu." alisema Salha.
![]() |
salha akiwa stejini akifanya yake |
![]() |
salha akiwa na mumewe Hammer Q katika pozi tofauti siku ndoa yao |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine