MAJARIBIO BLOG

Wednesday, July 24, 2013

FATUMA WA SEGERE AZIKWA LEO BAGAMOYO

FATUMA WA SEGERE AZIKWA LEO BAGAMOYO

Aliyekuwa mwimbaji wa wa kundi la Segere maarufu kwa kupiga nyimbo za kizaramo Fatuma Rajab atarajiwa kuzikwa leo katika kijiji  chao kilichopo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, imefahamika
Marehemu Fatuma Chuki aliwajibika akiimba huku akiwa amelala chini na mkononi kichwani
Akizungumza na mtandao huu Meneja wa bendi ya Segere bwana Masharubu alisema marehemu alifariki jana katika hospitali ya Muhimbili na alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kifua kwa muda yaliyopsababisha hadi jana kifukia umauti wake.



Marehemu Fatma wa mbele mwenye kaoshi ya chocolate akiwa katika ya pamoja na kundi la segere
 Mwimbaji huyo aliyekuwa machachari na mwenye ustadi wa kuimba nyimbo za kizaramo alipitia bendi mbalimbali lakini alipata maarufu zaidi pale alipoimba wimbo wa Segere namba mbili na kuchukua nafasi ya Siza Mazongela aliyekuwa amejiengua katika kundim hilo.

Inna lillah waina ilaihi raajiun.



No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine