MAJARIBIO BLOG

Wednesday, July 24, 2013

SIKO BENDII YEYOTE ILE - SABAH MUCHACHO

SIKO BENDI YEYOTE ILE - SABAH MUCHACHO

Mwimbaji nguli wa tasnia ya taarab nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla  Sabah Salum Muchaho amekana kuwa yeye si msanii wa kundi lolote la taarab, na kwamba yuko huru kufanya kazi sehemu yoyote endapo watamuhitaji kwa makubaliano maalum.

Akizungumza na Mtangazaji wa Kipindi cha Tam Tam za Mwambao Mwanne Othman kinacho ruka east africa radiopale alipokuwa akijibu swali ya kwamba yeye ni msanii wa kundi gani kwa imekuwa ikifahamika kwamba yeye ni msanii wa kundi la  5sats, ndipo alipojibu kwa herufi kubwa kwamba yeye si msanii  wa kundi lolote anafanya kazi popote atakapo hitajika tena kwa makubaliano maalim.

Sabah Muchacho akiwajibika

Hapa akitumbuiza harusini
 Bi Sabah alisema yeye ni mtu anayejishuhulisha na biashara kwahiyo hawezi kujifunga na bendi fulani kwasababu kipaji chake ndicho kinachompatia riziki kwahiyo hana budi kufanya kazi na vikundi mbalimbali ili aweze kujiingizia kipato.

Aidha alipotakiwa kujibu swali kuhusu kuingia mitini pale anapokuwa ametangazwa kuwepo kwen ye shoo alisema kuwa yeye ni mwenye kutegemea kipaji chake na endapo mtu atamtangaza kuwepo kwenye shoo bila makubaliano maalum basi hatoweza kuhudhuria kwenye hiyo kwakuwa hakukuwa na makubaliano yoyote ya awali.

"mimi nitakapotoka nyumbani kwangu kuja kenye shoo yako ndo usiku umeshaingia, sasa siwezi kuja kwa ajili ya kukufurahisha wewe muandaaji halafu nikitoka hapo mimi napiga miayo, kweli tangaza kwenye ma poster yako lakini sijii, kweli siji" alisema Sabah na kusisitiza.

Mwimbaji huyo mwenye watoto watatu  ambaye alianza muziki toka mwaka 1983 hadi sasa amepitia katika vikundi mbalimbali kikiwemo MAMESH, DUMBAKI, ALL STAR, EAST AFRICA MELODY,  ZANZIBAR STAR, NEW ZANZIBAR MORDEN TAARAB, huku akirekodi pia katika vikundi kama 5star na Gusa gusa Mini Band.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine