Kundi la Dar es Salaam Morden Taarab lililo chini Ukurugenzi wake Abdallah Feresh lenye maskani yake Magomeni Mtaa wa Tambaza liko mbioni katika ujio mpya ambao umeamua kuwazoa wasanii kutoka vikundi tofauti kuanzia waimbaji mpaka wapigaji kwa lengo la kuiimarisha zaidi bendi hiyo.
Akizungumza na Tam Tam za Mwambao mmoja wa viongozi wa kundi hilo ndugu Bakari Hassan alisema wameamua kuwachukua wasanii si kwa lengo la kutengeneza chuki baina yao na makundi mengine bali ni kuzidi kuliimarisha kundi hilo katika kazi zake.
Bakari alisema wameamua kuwachukua wapigaji kutoka makundi tofauti akiwemo Mpiga solo aitwaye Kisolo Ramadhan Mwana Malui na aliyetokea Mashauzi na Mgeni Kisoda ambao pia awali waliwahi kuwa katika Kundi hilo la Dar Morden kwa muda mrefu na baadaye kufukuzwa baada ya kutenda kosa la kurekodi wimbo nje ya bendi hiyo uitwao Chaja ya Kobe wa Mc Babu Ayoub kitendo ambacho hakitakiwi katika kundi la Dar Morden.
kwa upande wa waimbaji ni pamoja na Bi Mwanahawa Ally aka Chumvi, aka Jembe Gumu, aka Mtu mzima Kireja na tayari amesharikiodi wimbo wake uitwao siwanyimi uzuri, mwingine Mwamvita Shaibu aliyekuwa 5stars, Mosi Suleiman, Zubeda Mlamali, Hassan Vocha, pamoja na chipkizi wengine akiwemo Hasnat.
![]() |
Hassan Vocha akiwa na Hasnat |
![]() |
Bi Mwanahawa akiwa steji akifanya vitu vyake |
Mwamvita Shaibu akiwajibika |
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine