MAJARIBIO BLOG

Tuesday, February 4, 2014

DAR MORDEN KUZINDUA KITWITI NA OOH MY HONEY

Na Mwanne Othman

KUNDI la muziki wa taarab nchini Tanzania Dar Morden lenye maskani yake Magomeni jijini Dar es Salaam linatarajia kuzindua albam mbili kwa mpigo siku ya siku ya usiku wa Wapendanao kwa maana ya Februari 14 utakaofanyika katika ukumbi wa Tarveltine Hotel Magomeni.

akizungumza kwenye maskani ya bendi hiyo mmoja wa Viongozi wa Dar Morden Bakari Hassan alisema kuwa albam hizo zinakwenda kwa jina la Kitwiti itakayoimbwa na Sikudhani Ally na Oohh My Honey itakayoimbwa na mwimbaji wa Kiume anayechipukia katika taarab Hassan Vocha.

alisema albam hizo zote mbili zitakuwa ni moto wa kuotea mbali kwasababu zimesheheni nyimbo kabambe zilizoimbwa na waimbaji wazoefu na waachapaka akiwemo Mwamvita Shaibu alioimba wimbo uitwao Sikuamini macho yangu, mwingine ni Nakwenda kwa Mume wangu ulioimbwa na mwimbaji chipkizi Hasna Mlamali, Siwanyimi Uzur Bi Mwanahawa, Ngoma Imepasuka Hassan Vocha, na nyinginezo kama aliyoimba Zubeda Mlamali na Mosi Suleiman.

Alisema Uzinduzi huo unatarajiwa kusindikizwa na Baikoko pamoja na Kibao Kata.

Wasanii wa kundi la DAR MORDEN likiwa kazini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine