MAJARIBIO BLOG

Wednesday, January 1, 2014

KUMI WAZALIWA 27 WAJERUHIWA

Watoto Kumi wawili wakiwa wa Kiume na wa Kike wakiwa nane wamezaliwa  siku ya mkesha wa Mwaka Mpya  katika Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini, wakati huo huo Majeruhi 27 walifikishwa hospitalini hapo kwa ajali tofauti zilizotokea wakati wa Mkesha wa Mwaka Mpya.

kwa mujibu wa Afisa Muuguzi Kiongozi wa Zamu Bi Mary Shayo alisema Majeruhi hao wengine walifikishwa hospitalini hapo kutokana na ajali na wengin e waliookotwa na askari, ambapo majeruhi sita walifikishwa hospitalini hapo na skari ambao wameokotwa maeneo tofauti.

gari aina ya Vitz ikiwa shagalabagala baada ya kutokea ajali
Bi Mary alitoa ushauri kwa jamii kutafuta njia mbadala ya kusherehekea na kutnywa Pombe kupita kiasi kwasababu  asilimia kubwa ya majeruhi waliofikishwa ni wale ambao ajali zao zimesababishwa na Ulevi ama unywaji pombe kupindukia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine