MAJARIBIO BLOG

Tuesday, February 4, 2014

NIMEZOEA NYAMA NIKIPEWA DAGAA NAKIMBIA - BI MWANAHAWA ALLY

SIKUDHANI- SIWAHOFII WASANII  WALIOONGEZWA

MWAMVITA SHAIBU- NAMI PIA NIKIWEKWA NAKAA KAMA BI MWANA

 Na Mwanne Othman

MWIMBAJI nguli kwenye tasnia ya taarab nchini Bi Mwanahawa Ally amesema amezoea nyama kwahiyo siku atakayopewa dagaa hawezi kukaa kwa mume.

akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi cha taarab cha  Tam Tam za Mwambao kinachorushwa na east africa radio  Mwanne Othman pale alipoulizwa iwapo atadumu katika kundi hilo ama laa kwasababu umezoeleka kuwa Bi Mwanahawa si mkaaji katika makundi kwani amepitia takriban makundi yote makubwa na yenye majina kwenye tasnia ya  taarab sehemu nyingine akiondoka kwa amani na kwengine kwa tafrani za hapa na pale.

Mi nikiwekwa nakaa hata weee ukiolewa umezoeshwa nyama na mume wako siku ukiletewa dagaa utakaa? alihojoji Bi Mwana.

Akijibu kwa niaba ya Uongozi wa Dar Morden Bwana Bakari Hassan alisema kuwa anauhakikishia umma kwamba Bi Mwanahawa atadumun katika kundi kundi hilo kwani kiti chake tayari wameshakiwekea Superglue na wanaijua wao wenyewe, na kusisitiza Dar Morden haikuanzishwa kwa pesa za msimu hivyo ikipata ikikosa wasanii bado watapata haki zao.

naye kwa upande wake Mwamvita Shaibu alisema amejipanga vizuri kuwapa raha wapenzi wa Dar Modern hivyo wakae mkao wa kula.

Wakati huo huo Sikudhani Ally alisema hashitushwi na ujio huo wa wsanii wapya kwani wao watabaki kuwa wao na yeye Sikudhani atabaki kuwa Sikudhani na kila mtu atapata wimbo wake kwa wakati na ameahidi atafanya nao kazi vizuri.

Bi Mwanahawa katika pozi

Mwamvita Shaibu akiwa stejini akiimba

SIKUDHANI ALLY AKIWA STEJINI



No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine