Na Mwanne Othman
Diwani
wa kata ya Magomeni ndugu Julian Bujugo ametoa msaada wa chakula
jumla ya magunia 40 ya unga kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa
mafuriko wanaoshi katika mtaa wa Sunna Magomeni jiji Dar Salaam.
Akizungumza
wakati akiwasilisha msaada huo kwa niaba ya Diwani, Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa huo wa Sunna ndugu Alex Albert alisema anamshkuru
Diwani wao kujitolea lakini pia bado wanahitaji misaada zaidi ya
chakula ili waweze kujikwamua katika kipindi hiki kigumu
walichonacho.
Naye
mmoja wahanga hao aliiomba Serikali kufanya upanuzi wa Mto Msimbazi
sambamba na Mifereji mikubwa hadi baharini ili kunusuru makazi ya
watu ambayo yamekuwa yakiathiriwa na mafuriko.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine