MAJARIBIO BLOG

Monday, April 14, 2014

WAHANGA WA MAFURIKO WAIOMBA SERIKALI IWATAZAME KWA JICHO LA TATU

Na Mwanne Othma
14/4/2014

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imewataka wahanga wote wa mafuriko walioweka makazi yao katika Vituo vya mradi wa mabasi yaendayo kasi waondoke katika maeneo hayo.

Akizungumza na mwa4othman.blogspot.com, Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Sebastian Mhohela alisema wahanga wote wanatakiwa kuripoti katika ofisi za Mtendaji kata ili kupata maelekezo wapi waende.

Aidha Akizungumzia juu ya Maafa na madhara yaliyopo katika Manispaa ya Kinondoni yaliyotokana na mvua hizo alisema tayari idadi ya vifo vimeshafikia watu 24, miundo mbinu imeathirika kwa kiasi kikubwa kama maraja kuvunjika barabara kubomoka, na hata wanafunzi kukosa masomo kutokana na baadhi ya mashule kujaa maji.

mwa4othman.blogspot.com, ilizungumza na wahanga hao ambao nao waliiomba serikali kuwasaidia badala ya kutoa kauli za kuwataka kuondoka maeneo hayo.

Katika hatua nyingine mlezi wa Chama Cha Mapinduzi na Mchumi
wa tawi la tambaza ambaye pia ni mtoto wa Waziri wa Jinsia Wanawake na watoto Mh. Sofia Simba, aliyefahamika kwa jina Aladin ambaye alifika mahali hapo kuwapatia msaada wahanga hao kama maji, soda, mikate, mchele na kadhalika, alitoa wito kwa Serikali kuwatengenezea mazingira mazuri wahanga hao kwa kudhibiti mkondo wa maji ili waweze kuendeleza maisha yaoNaye


Mtangazaji wa east africa radio Mwanne Othman aliyeoneshwa kuguswa na hali ya wahanga hao hususan watoto wasio na hatia kupata tabu, hivyo aliamua kuwapelekea vitafunwa kama vile Mikate, Maandazi, Keki na kadhalika.


























No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine