MAJARIBIO BLOG

Monday, May 19, 2014

ADAM KUAMBIA KUZIKWA MAKABURI YA KINONDONI

Msanii wa filamu nchini Tanzania  Adam Kuambiana aliyefariki jumamosi ya mwishoni mwa wiki hii, anatarajiwa kuzikwa siku ya jumanne katika makaburi ya Kinondoni yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi ndugu Kaftany ataanza kuaga kuanzia saa 8 asubuhi katika viwanja vya leaders club na baada ya kumalizika shuhuli za kuagwa atazikwa katika makaburi ya Kinondoni.

Msiba kwa sasa uko Bunju B nyumani kwao na marehemu hivyo watanzania tujitokeze kwa wingi katika kumsindikiza mwenzetu hadi kufika safari yake ya mwisho.

Innalillah wainna ilaihi raajiun.


Adam Kuambiana enzi za uhai wake
 

 

No comments:

Post a Comment

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine