ATARAJIWA KUHAMISHIWA WODI YA UTAPIAMLO
Na
Mwanne Othman
Mtoto
aliyetelekezwa huko Morogoro kwa kuweka ndani ya boksi kwa takriban
miaka minne anaendelea vizuri katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es Salaa ambapo alifikishwa juzi usiku wa saa 3.
Mwanneothman.blogspot.com leo
ilitembelea hospitalini hapo katika jengo la watoto wodi B ambapo
ndipo alipolazwa na mtoto huyo na ilipata nafasi ya kuzungumza na Bi
Josephine Joel mlezi wa mtoto huyo aliyejitolea kuja nae Dar es
Salaam kwa kumpa malezi stahiki, na hapa anaeleze jinsi gani aliweza
kumpata mtoto huyo na kuambatana nae hadi Hospitali ya Muhimbili.
Mwanneothman.blogspot.com
ilizungumza na Muuguzi Kiongozi wa wodi hiyo aliyolazwa mtoto huyo Bi
Clara Moses ambaye alisema hali aliyokuja nayo tofauti na ya
sasa lakini tayari wameshachukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi zaidi
na leo hii wanatarajia kumuhamishia katika wodi ya Utapiamlo kwa
ajili ya kumpatia lishe zaidi.
![]() |
mtoto nasra akiwa amekalishwa juu ya meza |
Hatukuishia
hapo pia tulizungumza na wananchi wao kama wazazi wanakizungumziaje
kitendo alichofanyiwa mtoto huyo nao ni Katibu Muhtasi wa hospitali
ya Muhimbili Bi Jane Mahona na
Bwana Abdallah Muhoga mmoja wa kitengo cha Bohari ya dawa
hospitalini hapo ambao nao walisema wamesikitishwa sana na kitendo
cha unyama aliofanyiwa mtoto huyo.
Mwanneothman.blogspot.com
haikutaka kujiridhisha tu kwa kusikia kwamba mtoto huyo anaweza
kuongea hivyo ilitumia fursa pekee ya kuweza kuzungumza na mtoto huyo
ambaye ilimchukua muda mrefu kujibu pindi alipokuwa akiongeleshwa
lakini hatimaye alikweza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa kama vile
unaitwa nani, umekunywa nini leo akajibu maziwa amekupa nani bibi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine