MAJARIBIO BLOG

Wednesday, July 10, 2013

AROBAINI YA MUME WA KHADIJA KOPA JUMAMAMOSI HII

AROBAIONI ya aliyekuwa Diwani wa kata ya Magomeni wiliya ya Bwagamoyo Mkoa wa Pwani Jafari Ally ,ambaye pia aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki Khadija Omar Kopa, inatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 13 mwezi 7 mwaka huu.

Marehemu Jafari Ally enzi za uhai wa wake akiwa na mkewe Khadija Kopa siku ya ndoa yao.
 Akizungumza kwa njia ya simu Mwandishi wa Habari hizi, kaka wa maerehemu Idd Majid Rais wa Mtogole alisema arobaini hiyo inatarajiwa kufanyika nyumbani kwa Marehemu huko Magomeni wilaya Bagamoyo Mkoa pwani ambapo itatanguliwa na kisomo cha kumkumbuka marehemu na daada ya kisomo watalisha. 

Idd Majid aliwataka ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wakiwemo wadau mbalimbali wa taarab kuhudhuria katika arobaini hiyo ili kufanikisha shuhuli nzima ya kulisha.

Marehemu Jafari Ally alifariki dunia mnamo mwishoni mwa mwezi wa tano na akisumbuliwa na maradhi ya malaria na alizikwa katika makaburi yaliyopo Magomeni wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, huku akimuacha Mkewe Kipenzi Khadija Kopa kwenye EDA, akiwa katika wakati Mgumu wa kumkosa mumewe kipenzi.

2 comments:

  1. pole bi khadija utazoea tu pole sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. muda ni saa ngapi maana ukizangatia huu ni mwezi mtukufu wa ramadhani

      Delete

Tafadhali Ndugu Msomaji Zingatia Kutumia Maneno mazuri na ya busara kwa Faida ya Wasomaji Wengine